Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’.
Akizungumza hivi karibuni, Anti Lulu alisema sasa hivi
amejipanga kuyaendesha maisha yake kihalali na kwa kiasi kikubwa
amefanikiwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wanaotaka kumrudisha
nyuma.
“Watu wameniibia dukani kwangu ili kunirudisha nyuma lakini wamenoa,
sirudii zama za kujiuza tena. Duka nimeshalijaza, nimenunua kiwanja huko
Bunju na muda si mrefu nitaanza kujenga.
“Niwashukuru sana waandishi wa habari kwa kunibadili tabia kwani
huenda mpaka leo ningekuwa nafanya mambo ambayo hayana tija kwenye
jamii,” alisema Anti Lulu.