MBALI
na mtu mmoja kufariki dunia na wengine 24 kujeruhiwa na kulazwa kwenye
Hospitali ya Bwagala, Turiani mkoani hapa, mwanaume mmoja amekatwa nyeti
zake katika mapigano ya wakulima na wafugaji Jumanne iliyopita.
Mapigano
hayo yaliyoshuhudiwa na mwandishi wetu yalipoteza amani iliyokuwa
kwenye Kijiji cha Dihombo Kata ya Hembeti Wilaya ya Mvomero.
Mashuhuda
kadhaa walimwambia mwandishi wetu kwamba, mtu aliyekatwa nyeti
alikutana na wakulima hao wenye hasira waliokuwa wakimvamia mgeni yeyote
waliyemuona mbele yao.
“Wakulima
walikuwa na silaha za jadi kama vile mapanga, mishale ya sumu na
marungu, walimkuta mtu huyo aliyekuwa akipita na kumvamia kisha kumpiga
na alipoanguka chini mkulima mmoja alimkata nyeti zake,” alisema shuhuda
aliyejitambilisha kwa jina la Kibwana.
Mtu
aliyekatwa nyeti (angalia picha ukurasa wa mbele) hakufahamika jina
lake mara moja, lakini baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema
kwamba alikimbizwa hospitali ili kunusuru maisha yake.
Hata hivyo, baadhi ya wakulima nao waliumizwa vibaya katika tukio hilo lililosababisha kifo cha mfugaji Yusuf Mdutu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea
kwa mapigano hayo huku akisema kuwa msako mkali unaendelea kuwakamata
wahusika.
0 comments:
Post a Comment