Tuesday 31 December 2013

HII NI KUFURU....SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA MAGARI YA KIFAHARI TOKA SERIKALI YA CHINA,..WADHANI YANA TIJA KWA TAIFA?!!!

Serikali ya China imeipa serikali ya Tanzania magari ya kifahari aina ya Limousine, magari madogo na mabasi yenye choo na chumba cha mikutano kwaa jili ya viongozi. Msaada huo thamani yake ni mabilioni ya shilingi.

Kwa wenye kutafakari mambo kwa kina huu ufadhili ni dhihaka kwa wananchi wa tanzania na ni neema kwa viongozi, sikuzote wananchi wa tanzania tumekuwa tukijaribu kupunguza gharama za matumizi hasa magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali ilihali jamii inakosa huduma muhimu.
Naamini mfadhili hawezi toa ufadhili tuu bila mahitaji ya kinachotolewa.
Inatia shaka sana zawadi hizi sura yake imeekaaa kifisadi, fisadi, inatia shaka hasa kila kukicha unasikia wachina wamekamatwa na meno ya tembo, je hii ndio namna ya kutulipa watanzania kwa misaada isiyo na tija????
WATANZANIA TUTAFAKARI KWA PAMOJA HAPA.
SHUKA HAPO CHINI UTOE MAONI YAKO TAFADHALI.. 
Source: Jamii Forums

0 comments:

Post a Comment