Tuesday, 29 October 2013

JELA INAMUITA CHRIS BROWN.HUENDA AKAENDA JELA MIAKA MINNE.

Kwa mujibu wa TMZ Chris  na mlinzi wake walikamatwa jumapili asubuhi, na kwamba Chris alimpiga ngumi usoni mtu huyo majira ya saa kumi na nusu alfajiri nje ya hotel baada ya kutokea hali ya kutoelewana kati yao.
Mtu huyo aliyepigwa na Chris aliiambia TMZ kuwa ngumi ya Chris imepasua pua yake na inambidi leo (jumatatu) aende hospitali kufanyiwa upasuaji.
 Amesema yeye sio shabiki wa Chris na alikuwa anawapiga picha wasichana wawili ambao walikuwa wanapiga picha mwimbaji huyo nje ya hotel, na haelewi ni kwa nini Chris alikuwa kichaa vile na kumshambulia.
Hata hivyo mtu huyo amesema angeweza kumsamehe Breezy kama angeomba msamaha pale pale, lakini sasa hivi atamfunguliaa kesi dhidi yake na tayari ameshampata mwanasheria.
Lakini chanzo ambacho kiko karibu na Chris Brown kimesema kuwa mtu huyo hakuwa anataka kupiga picha nje ya hotel, bali alikuwa anataka kuingia kwenye ‘tour bus’ ya Chris ili apige picha akiwa ndani, na mwimbaji huyo alikuwa anajaribu kumzuia.
Kwa mujibu wa sheria za Washington, D.C, endapo Chris atapatikana na hatia anaweza kufungwa jela miaka minne.
Tukio hili linamuweka matatani zaidi mwimbaji huyo ambae bado yuko katika probation ya adhabu aliyopewa baada ya kumpiga mpenzi wa zamani ‘Rihanna’mwaka 2009.
Hii inaweza kutumiwa na mahakama kuwa Breezy amekiuka masharti ya probation hiyo.

0 comments:

Post a Comment