Kitaani huyu dogo anajulikana kama dogo ismail, ni maarufu sana mtaani
kwao huko Yombo. Dogo Ismail anishi na mzazi wake mmoja wa kike huko
Yombo na mama yake anafanya kazi kwenye kampuni fulani ya usafi hapa
jijini.
Dogo Ismail amemaliza darasa la saba mwaka huu 2013, huko huko Yombo
alipokuwa akiishi yeye na mama yake, lakini dogo huyu anasifa yake moja
kuu ya ugomvi. Wakati akiwa bado shule alikuwa akiwaletea sana utata
walimu na wakati mwingine hata kushikana mashati na kupigana, alishawahi
kumpiga jiwe mwalimu mkuu akiwa mstalini, dogo alirudishwa nyumbani kwa
muda fulani na baadae alirudishwa shule, Mama yake Bi. Mariam
akiendelea kuileza The ClickTz:
Mtoto wake alidhaniwa kuwa labda anamatatizo ya akili, lakini yeye
mwenyewe anakanusha huku akisisitiza kuwa mwanae yuko sawa kabisa ila ni
utoto tu kwani wakati mwingine watoto huwa hivyo na wanapokuwa
hubadilika na kuwa wema kabisa, na akiongezea kuwa Ismail anapo kuwa
nyumbani ni mtulivu sana hivyo anashangaa matukio anayoyafanya huko
nje.!!
Kwa mujibu wa watoto wenzake wa kitaa wanadai kuwa Ismail ni mgomvi
sana, na huwa anashindaga kwenye kibanda fulani cha video hapo kitaani
mara tu anapotoka shule na kurudi nyumbani kwao jioni hivyo labda huko
ndiko anakopata maujuzi ya ugomvi na kujifanya stelingi wakati wote.
0 comments:
Post a Comment