Wednesday, 13 November 2013

NIMEGUNDUA MCHUMBA WANGU KATOA PENZI KWA MTU MWINGINE...!! USHAURI JAMANI NIFANYEJE...??




Wadau wa MAVITUZI BLOG naombeni ushauri wenu kijana mwezenu yamenikuta, mimi nina girlfriend tangu mwaka jana, nimekuwa nikimpa support ya shule kama ada na mahitaji mengine kadri ninavyoweza. 

Mwaka jana aliombwa na dada yake akampe campani huko mbagala kwaani alikuwa amepata motto mchanga. Tangu aende kuishi kwa dada yake alianza kubadirika katika mawasiliano, aliniambia kuwa hakuwa free kama alipokuwa kwa wazazi wake temeke. 

Kwaani kila nikimhitaji ilkuwa ni ngumu au kwa nadra sana mfano tuliweza kuonana mara moja kila baada ya miezi 1-2. Mawasiliano yetu makubwa yalikuwa ya simu. Kwa sababu ya mawasilano yetu kuwa finyu tuliweza kutofautiana mara kwa mara hivyo hata ile support yangu ikawa inapungua kwa sababu ilikuwa ni lazima niende kwenye tigopesa kumuwezesha nayopia ilitegemea nimepata muda gani kulingana na mazingira ya kazi yangu.

Bahati nzuri mpenzi wangu amerudi nyumbani kwa wazazi sasa yapata mwezi mmoja na tunaweza kuonana mara kwa mara na mahusiano yetu yamestawi vizuri tena. Kwa bahati mbaya juzi siku ya Eid simu yangu nilimwazima mdogo wangu alikuwa amepoteza simu yake huku akiwa na issue ya pesa. 

Hivyo mpenzi wangu hakuweza kunipata alichukia sana mpaka akawa hapigi simu wala hajibu sms zangu kwa muda wa siku 3. Jumatatu wiki hii baada ya kazi nilienda kujua kulikoni, aliponiona tu aliniambia nimefuata nini? Nilimshangaa sana, akasema kuwa najifanya sijui kwa nini sikupokea simu yake siku ya Eid.

 Nilimwelewesha na kumwomba msamaha. Baadae nilimuuliza kuwa nilikuwa nimeona gari pale nyumbani kwao na nikajifanya kama nimepata taarifa kuwa ni ya mtu wake, alinijibu kuwa kwa hiyo nina amuaje..?? 

Niliamua kuchukua simu yake kwa nguvu nikaondoka nayo. Usiku iliingia sms iliyikuwa inamtaka wakafanye mapenzi kwaani ilikuwa yapata miezi 4 tangu wafanye mala ya mwisho. Sikuamini nilichokiona. 

Jana jioni nilienda kukutana nae na kumuuliza kuhusu sms hiyo alilia na kuomba nimsamehe kwani alifanya mara moja kwa kuwa hatukuwa na mawasiliano mazuri kipindi hicho akiwa Mbagala eti alihisi tulikuwa tumeachana na alikuwa na shida ya shule hivyo ilimbidi kumkubali mtu bila kupenda. Zaidi aliniambia kuwa mbona yeye alinisamehe mwaka jana alipopata ujauzito tukautoa hata bila ya wazazi au dada yake kujua? Ni kweli tulitoa mimba ya mwezi 1.5. Lakini tulishauliana kuwa asome kwanza hayo mengine ndiyo yafuate. Akakubari.

Wadau naombeni ushauri wenu nifanyeje kijana mwenzenu yamenikuta na binti nampenda lakini kwa sababu ya hili la kutokuwa mwaminifu nimemwambia kuwa tangu jana tumeachana, kiukweli usiku kucha sijapata usingizi hata dk 1. Hapa nilipo nawaza sana. Na yeye ananiomba msamaha hatarudia ilitokea bahati mbaya.


0 comments:

Post a Comment