TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr Sengoondo Mvungi ambacho kimetokea katika hospitali ya Millpark nchini Afrika kusini.
Uongozi wa UVCCM Taifa unatoa pole kwa familia na ndugu wa marehemu, pia UVCCM inatoa pole kwa uongozi wa NCCR- Mageuzi na kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Warioba pamoja na Vijana nchini kote ambao wamenufaika na Utaalamu na mafunzo.
Kama
vijana tulihitaji sana mchango wa mawazo, hekima na utaalamu kutoka
kwake, hakika tumepoteza kiongozi shupavu, muadilifu na mzalendo ambao
ni mfano wa kuigwa kwa Vijana wa Taifa hili.
Kadhalika, UVCCM inatoa pongezi za dhati kwa hotuba makini iliyojaa hekima, busara na ushupavu wa Uongozi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Pia,
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesikitishwa na tuhuma
ambazo zimeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kutoka kwa
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mheshimiwa Godbless Lema ambazo
amezielekeza kwa baadhi ya Viongozi wa Jumuiya akiwemo Mwenyekiti wa
Taifa wa UVCCM Ndugu Sadifah Juma kuwa amehusika na usambazaji wa Picha
chafu za uchi mitandaoni.
Pamoja na kusikitishwa, UVCCM inazo taarifa juu ya mgogoro unaoendelea katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kwamba inamtaka Lema kutoelekeza tuhuma kwa UVCCM na viongozi wake bali waangalie namna bora ya kushughulikia na kutatua migogoro yao ya ndani ambayo imesababisha kuzushiana, kuchafuana na kuvujishiana siri katika mitandao ya kijamii.
UVCCM na Viongozi wake inakana kwa namna yeyote ile kuhusika na usambazaji huo na kwamba Jumuiya hii ni ya Vijana makini na wanaojitambua na inajielekeza katika kufanikisha malengo ya kuundwa kwake ya kukisaidia Chama kushika dola mwaka 2015.
Na kwamba UVCCM inalaani tabia ambayo imeasisiwa na Vijana wa CHADEMA ya kukashifu, kuzomea na hata kutukana Viongozi wa CCM na Serikali yake na kwamba yaliyomkuta Mhe Lema ni matunda ya kazi waliyoiasisi wenyewe.
Imetolewa na:
PAUL MAKONDA
KATIBU WA IDARA YA HAMASA NA CHIPUKIZI
UVCCM
13/11/2013

0 comments:
Post a Comment