Friday 6 December 2013

ANTI LULU ATUNDIKWA MIMBA..


baada ya kurukaruka sana, sasa inadaiwa ni
mjamzito wa takribani miezi mitano.
Akilinyetishia Ijumaa juu ya ishu hiyo, rafiki wa
karibu wa Anti Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake
alisema, msanii huyo sasa amekuwa mtumiaji
mzuri wa maembe mabichi huku magauni
mapana yakiwa ndiyo mavazi yake.
“Mwanzo alikuwa anaficha lakini sasa siyo siri na
mwenyewe ameona ni bora kuwataarifu ndugu na
marafiki zake,” alisema mtoa habari huyo.
Katika kujua undani wa hilo, waandishi wetu
walimsaka Anti Lulu na kufanikiwa kumuona
akiwa na kitumbo chake lakini akaomba asipigwe
picha ila akasema: “Mmechelewa kujua, mbona
inakwenda mwezi wa tano sasa, mwenye mzigo
mtamjua nikishajifungua jamani,”alisema msanii
huyo.
GPL
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya

0 comments:

Post a Comment