Wanausalama wakipanda juu ya mnara kumnusuru jamaa huyo.
Jamaa huyo akiwatuhumu polisi kwa kuwabambikiza kesi wananchi wakati akiongea na wanahabari baada ya kushushwa kutoka kwenye mnara.
Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na polisi.
Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi ashijirushe na kufanikiwa kushuka naye.
(PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
0 comments:
Post a Comment