Wednesday, 4 December 2013

MKASA WA KWELI : SERENGETI BOI AJIUA BAADA YA KUTOSWA NA SHUGA MAMI WAKE NIGERIA.

Kijana mmoja kutoka Nigeria aliyefahamika kwa jina la Michael Jaja(22) ameamua kujirestisha In Peace baada ya mwanamke aliyekuwa akimlea wanaofahamika kwa jina la shuga mami(48)  kumtaka wavunje uhusiano wao kutokana na ujio wa ghafla wa  mume wake ambaye alikuwa akiishi nje ya nchi kwa miaka kadhaa.

Katika Picha ni Michael Jaja na Mwanamke aliyekuwa akimpa jeuri (Shuga mami) wakila bata Dubai.
Chanzo kimoja cha habari kutoka Nigeria kilieleza kwamba Jaja alikuwa ameshazoea maisha ya raha na starehe aliyokuwa akipewa na mama kubwa huyo mpaka kufikia hatua ya kununuliwa gari ya kutembelea aina ya Toyota Corolla kama zawadi sambamba na safari za kwenda Dubai na China kula bata vilevile kuishi katika jumba la kifahari la mwanamke huyo aliyekuwa akimpa jeuri mjini.
Baada ya mwanamke huyo kumwambia waachane kutokana na ujio wa mume wake huyo, Jaja alitishia kumuua na kujiua kama ataachwa kutokana na kufikiria kurudia katika hali yake ya  msoto kama zamani, habari zinasema kwamba walipokea taarifa za mtu kujiua kwa kitu kinachodhaniwa ni bastola na ndipo ripoti za polisi zilipobainisha kuwa aliyekufa alikuwa ni Michael jaja na hata baada ya mwanamke yule alipoenda kutoa salamu za pole kwa mama aliyetambulishwa kuwa ndiye mkwe wake aliambiwa kwamba alidanganywa na kijana huyo, hii sio mara ya kwanza kwa vijana wa Nigeria kuamua kujiua kutokana na mikasa kama huu uliomtokea Jaja.
Credit-Larrybway91

0 comments:

Post a Comment