Wednesday, 13 November 2013

PICHA YA DIAMOND PLATNUM AKIWA AMEVAA BOKSA TU


Wewe ni mkari tena sana ndio nakubali,Napenda jitihada zako katika kazi,Mimi ni shabiki mzuri tu LKN KWA HILI DIAMOND HATUPO PAMOJA.Leo katika Ukurasa wake wa Facebok msaniii Diamond Platnum ametupia China inayomuonesha akiwa amevalia Boksa huku akiwa kifua wazi akiendelea na harakati za kuaanda chakula akiwa Nchini Nigeria.

Natambua Diamond unatambua kuwa wewe ni kioo cha Jamiii na kuna watu wengi wanafanya mambo ambayo wanaiga kutoka kwako kwa kuwa wamekuona wewe ukikifanya na kuona kuwa wako sawa katika Jamiii ili hali hicho kitu hakina Usawa katika Jamiii yetu ya Kitanzania.

Natambua kuwa Tamaduni za Wenzetu zinaruhusu mtu kufanya kile akifanyacho katika kujitangaza kibiashara na kuzidi kujipatia jina kubwa kutokana na matukio hayo wanayokuwa wakiyafanya kila siku katika maisha yao ya kila siku lkn Kwetu sisi Tunatamuduni zetu ambazo zinapaswa kulindwa na kufuatwa.

Nimesema wazi kabisa kwa hili sikuungi mkono kabsaa kwani natambu madhara ya vitu unavyovifanya katika Jamiii hivyo hiki unachotaka kukufanya au unachokifanya hata kama ni biashara lakini jaribu kuangalia Tmaduni zetu zinasemaje na ujaribu kuziheshimu.

Nakubali sana Uwezo wako katika kazi zako na jitihasa zako katika kuufikisha muziki katika Ngazi kubwa zaidi kama ambavyo kwa sasa unafanya kwakuwa jina lako ni kubwa na linazidi kukuwa zaidi jaribu ku protect Image ya Brand yako maana Umefanikiwa kujitengenezea Brand hivyo unapaswa kuulinda na kuiheshimu itakusaidia.

Imani yangu ni kwamba unaweza kufika mbali kutokana na Sauti yako na Lugha yako ya Kiswahili ambayo inaladha ya kiswahili hivyo simamia hicho ilikufika mbali zaidi kisanaa kwani Tukisema Swaga huko mbele kuna swaga teyari,na kama tukisema mavazi bhasi huko mbele teyari kuna Mavazi ya dhamani so Mtaji wako mkubwa ni aina ya muziki unaoufanya na Sauti zako ambazo zimekuwa zikiwachanganya Wana Afrika Mashariki na Kati.

Muda mwingine angali maana hakuna kitu kikubwa wala kidogo inapokuja katika suala la kulinda Image Yako na Brand Yako,muda mwingne acha vitu vipite tu na usiwape nafasi watu kuanza kukuzungumzia vibayaa maana utakuja kutumia Gharama kubwa katika kuja kusafisha Brand yako wakati mwenyewe ndiye uliyechangia kuibomoa.

0 comments:

Post a Comment