Staa wa sinema na
muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan
Ngassa wamenaswa ‘laivu’ wakiwa kimahaba......
Kwa mujibu wa
mnyetishaji wetu, tukio hilo lililijiri hivi karibuni nyumbani kwa Snura maeneo
ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao walibambwa wakiwa
wamejiachia ‘wakifanya yao’.
Mnyetishaji huyo
alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa
wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.
“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Baadaye hata
Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,”
alidai shuhuda wetu.
Ili kujiridhisha, Tulisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu
zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua utata na maswali kwa
walioziona.
Uchunguzi
ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura na Ngassa kunaswa wakiwa beneti
kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini
Dar wakila bata ndefu.
Baada ya kulishwa
‘niuzi’ hizo,Tulimsaka Snura ambapo alipopatikana alitakiwa
alimwagiwa habari yote juu ya uhusiano wake tata na Ngassa ambapo alikuwa na
haya ya kusema:
“Nimeshtuka sana
kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye
(Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu.
Ngassa na Snura ndani ya pozi tata.
“Ngassa
alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu
ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”
Kwa upande wake
Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa Ligi
Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila
kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment