Shabiki maarufu wa Yanga Steven amejitosa katika fani ya filamu ambapo ataanza kuonekana karibuni akiwa katika muvi inayoandaliwa na Dr Cheni itayokwenda kwa jina la 'Nimekubali Kuolewa'.
Steven alijipatia umaarufu ghafla baada ya mitandao kurusha
video inayomwonesha analia baada ya timu ya Yanga anayoishabikia
kufungwa.
Kwa upande wa Dr Cheni ambaye ni msanii aliyeanza fani hii
takriban miaka 15 iliyopita, anakuja kiviungine baada ya kukaa kando kwa
mwaka mmoja.
Katika filamu hii pia kuna nyota kutoka China ambaye
anakuwa Mchina wa kwanza kuigiza kwenye Bongo Movie.
Tazama moja ya scene ya filamu hiyo jamaa akimwaga chozi kama kawaida
0 comments:
Post a Comment