Wednesday, 13 November 2013

PICHA ZINAZOTHIBITISHA UMOJA NI NGUVU KWA WASANII KUFIKIA MAFANIKIO ZINAMUHUSU PROJ JAY -LADYJAYDEE,AY - FA


KATIKA PICHA HII ILIYOPIGWA MIAKAA KADHAA ILIYOPITA KUSHOTO PROF JAY KATIKAKATI lADYJAY DEE NA MWISHO KULIA NI MAC DIZOO.
Maisha ni Historia na mafanikio siku zote hayaji kwa njia nyepesi kama ambavyo wengi wetu tunafikiri au kudhania kwangu mimi maisha na mafanikio naona ni vitu
viwili vilivyotofauti lakini cha ajabu vinategemeana sana.

Kuna vijana wengi sasa wanataka kujilinganisha na Kaka Zao au wanataka kushindana na dada zao ingawa haikatazwi kushindana na inawezekana ukajiona umefanikiwa sana kwa Tafsiri yako ya Maisha ingawa kuna watu bado wanakuona unasubiri sanha kuwafikia hao watu kutokana na tasfiri yao ya Neno Maisha na Mafinikio katika Maisha.
LADYJAYDEE NA PROF JAY

Jaribu kujiuliza Mafanikio aliyonayo Mtu kama Prof Jay,Ay,FA ,Lady Jaydee Jumanuture,Diamond Platnum,Salama Jabir.Juma Kaseja,Fid Q,na watu wengine wengi kuwataja kwa majina halafu jiulize kitu kimoja Wamewekeza Miaka Mingapi kufika hapo walipo?

Uvumilivu+ Kujituma+Nidhamu=Mafanikio Lakini mafanikio mazuri zaidi ni pale unapowekeza nguvu binafsi na kushirikiana vizuri na wenzako na kuwa kitu kimoja.
AY AKIWA NA SWAHIBA YAKE FA MIAKAA KADHAA ILIYOPITA

Picha hizi zimepigwa na watu tofauti katika miaka tofauti lakini zilihusisha sura zilezile kwa miaka hiyo na hicho ndicho kilichofanya watu hawa kuweza fanikiwa katika kazi zao na kupata Matokeo makubwa ya Kazi zao.

Usiigee Matumizi Iga kazi na ifanye kazi zaidi yake Utatoka tu kwa namna moja au nyigine hawa watu wanapatana na kuendana na ndio maana miaka inapita bado wapo pamoja na wanazidi kufanya kwa kushirikiana kimawazo hata utendaji,ndio maana anachofanya mwingine mwenzake anaona moja kwa moja na yeye kinamuhusu,hivyo hawana usaliti wa kijinga kijinga au kukosa misimamo katika kile wakifanyacho.
AY NA SWAHIBA YAKE HIVI KARIBUNI




KATIKA KULIONA HILI SIJAZUNGUZIA MAFANIKIO YA KUNENEPA HAPA ILA KAMA MFUATILIAJI MZURI WA KIWANDA CHETU CHA MUZIKI NA KUJUWA HISTORIA YA MUZIKI WA BONGO UTAKUWA UNAJUWA NINI NAKIMAANISHA HAPA.

0 comments:

Post a Comment