Wednesday, 18 December 2013

UFISADI MPYAAA WA MWENYEKITI WA TAIFA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI, FREEMAN MBOWE WAANIKWA



Imeandikwa na 
Habibu Mchange
0762178678:
-------
 Juzi niliandika kuhusu unafiki wa MBOWE kuwahadaa Watanzania ya kwamba yeye hanunuliki, nilitoa ushuhuda wa MBOWE kupokea million 100 kutoka kwa ROSTAM AZIZ aliyekuwa mwanamkakati muhimu wa ushindi wa Urais kwa mgombea wa CCM mwaka 2005 Mheshimiwa JAKAYA KIKWETE, ambapo pesa hizo zilipokelewa mwezi oktoba 2005 na kumfikia mbowe kupitia kwa mke wake ndugu LILIAN MTEI MBOWE, na kumfikia MBOWE ambaye kipindi hicho alikuwa anagombea URAIS kupitia CHADEMA,

hapa mbowe sio tu kwamba alinunuliwa, alihongwa ama kutumiwa kuwadhoofisha wapinzani waliokuwa na nguvu kipindi hicho, bali pia alidhihirisha namna gani yeye ni mpinzani mtiifu kwa CCM (alikubali kutumika) na ni MNAFIKI ALIYETUKUKA.

Leo tarehe 18.12.2013, Magazeti kadhaa yameripoti juu ya muendelezo wa unafiki wa MBOWE na vibaraka wake.

Magazeti yameandika pamoja na mambo mengine, kwa ufupi kabisa hivi ifuatavyo.

• Amemshinikiza mbunge wa viti maalum ndugu JOYCE MUKYA kukatisha ziara ya kikazi za kibunge alipopangiwa na kumlazimisha wakakutane nyumbani kwake DUBAI, inawezekana ni kwenda kumlea motto wao FREELADY MBOWE, ama vinginevyo, lakini huu ni uthibitisho wa UNAFIKI wa MBOWE mbele ya WATANZANIA, kushiriki kutumia kodi za watanzania kwa matumizi binafsi tena ya KIMAPENZI na mwanamke aliyemteua kuwa mbunge bila ya kuwa na uwezo wa kukidhi vigezo vya uteuzi wa UBUNGE ndani ya chama. Kwa sasa JOYCE MUKYA ni mbunge, Hawara na mama wa motto mmoja aitwaye FREELADY MBOWE, Aliyejifungulia NEW YORK NCHINI MAREKANI kwa kutumia kodi za Watanzania.


• MFUASI WAKE ASIYEJIELEWA – JOSHUA NASSARY, wiki chache zilizopita mbunge huyu wa UPEPO WA CHAMA alishiriki kumtuhumu ndugu Zitto Kabwe Kuwa anasafiri nchi nyingi ili apate posho za safari, afadhali aliyemtuhumu kuwa anasafiri, lakini yeye ameumbuliwa kuwa AMESHIRIKI KUCHUKUA pesa za UMMA WA WATANZANIA, kisha kutokwenda kushiriki ziara ya kimafunzo kwa maslahi ya nchi. Million 8 alizopewa nassary si pesa nyingi kusema anaweza kutia hasara sana, lakini ni pesa zinazoweka rehani ule upambanaji anaojitambulisha nao mbele ya jamii, ni pesa zinazoweka hatiani uwajibikaji anaojitamba nao, ni pesa zinazomdhihirisha kwamba yeye ni mwizi wa mali ya umma kama walivyo wezi wengine.

UNAFIKI WA AWALI WA MBOWE NA WAFUASI WAKE.

• Walijitangaza hadharani kuwa Hawapokei na wanapinga posho, LAKINI MPAKA SASA WANARAMBA POSHO KAMA KAWAIDA, na pindi inapotokea imecheleweshwa kulipwa wanasimama kidete kuidai, mwanachadema pekee asiyepokea posho ni ZITTO KABWE.

• MBOWE, kwa mbwe mbwe kubwa alilirudisha gari la kiongozi wa upinzani, kwa nderemo, vigeregere, matarumbeta waandishi wa habari na vifijo, kuwa kutumia gari la KUB ni kuwakosea Watanzania, kuwadharirisha na kuzitumia vibaya rasilimali za Taifa letu, hapa mbowe akajidai ni mzalendo, tuliokuwa tunamfahamu tulicheka tukamuacha kama ataweza kuhimili alichokisema.

• MBOWE, kwa aibu kubwa, akajirudishia gari la KIONGOZI WA UPINZANI, hapa akatafuna matapishi yake mwenyewe, ila safari hii alifanya kimya kimya.

• Kwa masikitiko makubwa hivi sasa mbowe anashirikiana na watuhumiwa wengine wanaomiliki mali nyingi nje ya nchi ikiwemo uswiz na kwengineko. 

• Mbowe anamiliki NYUMBA TATU, Pesa na mali nyinginezo nje ya nchi, anamiliki NYUMBA – AFRIKA YA KUSINI , DUBAI NA MAREKANI. Ameshaitwa kuhojiwa namna alivyoweza kuzipata NYUMBA HIZO ama kama kuna biashara anafanya zaidi ya UMILIKI WA DANGURO LA BILLCANAS.

• Mbowe anawatetea watoto wa kimasikini wa Kitanzania, ili hali watoto wake wote sio Watanzania kwa Kuzaliwa, Mpaka sasa anajitamba kwenye vikao vya chama kuwa mtoto wake mmoja amezaliwa NEW YORK (Huyu ni mmarekani wa kuzaliwa), Mtoto wake Mwingine amezaliwa LONDONI huyu ni Muingereza kwa kuzaliwa , na motto wake wa sasa hivi aliyemzaa na JOYCE MUKYA amezaliwa NEW YORK (Huyu naye pia ni mmarekani wa kuzaliwa). Uzalendo wa MBOWE uko wapi mpaka sasa?.

UNAFIKI ZAIDI

Naomba nishirikiane nanyi kujiuliza maswali machache, UKO WAPI UZALENDO WA MBOWE?, 
Kuna Tofauti gani kati ya mali za Mbowe nje ya Nchi na Vijisenti vya Andrew Chenge?. Mbona hawa wote ni wamiliki wa mabilioni nje ya nchi?.

Uzalendo wa Mbowe unatokana na nini kwa Watanzania, kwanini Watanzania Tumpende Mbowe ambaye hatupendi?, hapendi shule zetu, Hapendi Hospitali zetu, hapendi ardhi yetu ndio maana anamiliki majumba nchi za nje.

Kwanini tusiamini mbowe anashiriki kutuchafua kama Taifa hasa vijana akijua kabisa watoto wake yeye sio Watanzania. Ina maana mbowe hapendi watoto zake waje kuwa viongozi wa Taifa hili kama ilivyo kwake?, kama la, kwanini amewanyang’anya haki ya wao kuwa watanzania wa kuzaliwa?.

Nimeamua kujitoa Muhanga kuwaelewesha masikini wenzangu, walalahoi wenzangu na wanyonge wenzangu, Mbowe sio mtetezi wetu, mbowe ni mfanyabiashara ambaye mtaji wake ni umasikini wetu, anatutumia sisi masikini na walalahoi kama mtaji wake wa kisiasa, anatutumia bila ya sisi kujijua, mbowe ni Tapeli wa kisiasa.

HISTORIA INAMPINGA

Mimi ni mkuumini wa Historia ya ukombozi, ninafahamu dunia nzima namna nchi zilizohitaji ukombozi namna zilivyopata ukombozi na namna ya viongozi wao waliowakomboa walivyojitokeza kwenye jamii.

Mbowe ndio mfanyabiashara pekee anayejiita mtetezi wa masikini duniani, tangu nimewahi kuifahamu historia ya ukombozi,

Hakujawahi kutokea Duniani labda ahera, Masikini wakatetewa na Tajiri, Haijawahi na Jaitawahi kutokea Mfanya biashara yoyote akapanga kupata hasarfa eti kwa maslahi ya Umma, wafanya biashara wote wanawaza faida, hata mbowe anawaza faida na sasa anatafuta faida kwa gharama yoyote.

Tunamsifia Mandela leo, Mandela hakuwa mfanyabiashara, Mandela hakuwa tajiri, Mandela alichangiwa na masikini wenzake kuikomboa Arika ya Kusini, Mandela hakuwahi Kuikopesha ANC pesa ili iwaondoe Makaburuu, Mandela alifanana na jamii aliyotaka kuikomboa na Mandela alifanikiwa kuikomboa.

Wote tunamsifia Nyerere Hapa Tanzania, Nyerere Hakuwa Mfanyabiashara, mwalimu Hakuwa Tajiri, mwalimu Hakuwahi kuikopesha TANU ili kumuondoa MKOLONI, nyerere alichangiwa na masikini wenzake, aliombewa na walalhoi wenzake na alilindwa na mafukara wenzake.

Mkifano ni mingi, hivyo hivyo kwa Samora Machel, Kwame Nkuruma, Milton Obote, Robert Mugabe, Kamuzu Banda, Dkt Martin Lutherking, Mahatma Gandh, Mao Zedong, AmilicaCabra na wengineo wote, KAMWE KUNGURU WASIOFANANA HAWAWEZI KURUKA PAMOJA.
Nitaendelea kuwafundisha mengi ninayoyajua kuhusu MBOWE NA CHADEMA kwa kadri itakavyowezekana.

Itoshe tu kusema kwa sasa kwamba Taifa letu kweli linahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala, linahitaji mabadiliko makubwa sana ya kisera kimfumo na kimuundo, na ni kweli kabisa CCM imeshindwa kuendana na Kasi hii ya uhitaji wa mabadiliko, lakini Bahati mbaya sana watu sahihi wa kufanya Mabadiliko bado hawaonekani, bado Hawapo, Bado wanafanyabiashara ya kisiasa.

TAHADHARI.
Nimekuwa nikipokea meseji za vitisho kupitia simu, email na facebook, kuwa nitauawa kama wangwe, ninasema hivi, nipo tayari kwa yote na mwenye uhakika wa kufanya hivyo asipate shida, anipigie simu kwa namba yangu 0762178678 NITAMFUATA ALIPO ATIMIZE LENGO LAKE.


Kwangu Daima NYEUPE NI NYEUPE na NJANO NI NJANO.
Mimi
Habibu Mchange
0762178678
mchangehabibu@yahoo.com

0 comments:

Post a Comment