MMOJA wa mawaziri wa Serikali ya Awamu
ya Tatu na mbunge anayetoka Mkoa wa Tabora, anatuhumiwa kumbaka na kisha
kutishia kumuua msichana yatima mwenye umri wa miaka 16 (jina
limehifadhiwa) anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni
jijini Dar es Salaam.
, |
Waziri huyo (jina lake linahifadhiwa kwa
sasa), ametoa tishio hilo la mauaji kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia
namba iliyosajiliwa kwa jina lake kwa kile alichodai kukaidi amri ya
kutaka wasifichue uchafu wake kwa waandishi wa habari.
Akizungumza kwa uchungu na mwanafunzi huyo alisema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012.
Mwanafunzi huyo alisema alifikwa na ukatili huo alipoitwa na kiongozi huyo kwenda kuchukua fedha za ada na matumizi mengine, ambapo mara ya kwanza alimpa sh 700,000 na mara ya pili sh 350,000.
Yatima huyo anayeishi na dada yake, alikutanishwa na waziri huyo wa zamani na baba wa mwanafunzi mwenzake, kutokana na msaada mkubwa aliompa akiwa mgonjwa, ili aweze kumsaidia fedha za ada kama ishara ya shukurani.
Mwanafunzi huyo alisema baada ya kutambulishwa, aliitwa katika hoteli hiyo ambako baada ya kufika mapokezi wafanyakazi walimkataza kuingia chumbani kutokana na umri wake kuwa mdogo (mwaka 2011 alikuwa na miaka 14), lakini waziri huyo wa zamani aliamrisha aruhusiwe...

0 comments:
Post a Comment